𝐑𝐚𝐢𝐥𝐚 𝐎𝐝𝐢𝐧𝐠𝐚 𝐚𝐰𝐚𝐡𝐢𝐦𝐢𝐳𝐚 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐤𝐮𝐳𝐢𝐧𝐠𝐚𝐭𝐢𝐚 𝐦𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝟒𝐑.

𝐑𝐚𝐢𝐥𝐚 𝐎𝐝𝐢𝐧𝐠𝐚 𝐚𝐰𝐚𝐡𝐢𝐦𝐢𝐳𝐚 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐤𝐮𝐳𝐢𝐧𝐠𝐚𝐭𝐢𝐚 𝐦𝐢𝐬𝐢𝐧𝐠𝐢 𝐲𝐚 𝟒𝐑.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameasa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wazingatie msingi mmoja wapo wa falsa ya 4R ambayo ni maridhiano.

Odinga amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X baada ya kutembelewa na viongozi wa juu wa Chadema akiwemo Mwenyekiti Tundu Lissu.

“Tulibadilishana mawazo kuhusu uimarishaji wa demokrasia katika bara hili, ikiwa ni pamoja na mchango madhubuti katika maendeleo ya taifa na vyama ndani na nje ya serikali” alieleza Odinga.

Aidha, Odinga alisema amewahimiza Chadema kutanguliza mazungumzo na ushirikiano wenye kujenga na Serikali kwa maslahi ya taifa na uhifadhi wa demokrasia ya Tanzania.

Viongozi wengine waliokuwepo ni Makamu Mwenyekiti Bara wa Chadema, John Heche na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.