Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imeunda tume ya kuchunguza yaliyotokea katika vurugu za Oktoba 29, mwaka huu ili kujua kiini cha tatizo.
Ameeleza taarifa ya tume hiyo, itaiongoza Serikali kujielekeza katika mazungumzo ya kuleta maelewano na amani.
Ameambatanisha hilo na kutoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu na jamaa walipoteza maisha katika tukio hilo, kadhalika kuwaombea wale waliojeruhiwa wapone haraka.
“Mimi binafsi nimehuzunishwa sana na tukio lile natoe pole kwa familia zote zilizopoteza familia zao na tunaomba Mungu azipumzishe roho zao kwa amani.
“Kwa majeruhi tunawaombea wapone kwa haraka na waliopoteza mali zao, tunawaomba wawe na stahamala na uvumilivu,” amesema.
Mkuu huyo wa nchi ameyasema hayo leo, Ijumaa Novemba 14, 2025 alipotoa hotuba ya kulifungua Bunge la 13, jijini Dodoma.
