KATIKA MAZINGIRA HAYA TUNDU LISSU ANA HAKI YA KUCHANGANYIKIWA.

KATIKA MAZINGIRA HAYA TUNDU LISSU ANA HAKI YA KUCHANGANYIKIWA.

Fikiria umeshinda nafasi ya Mwenyekiti wa chama cha siasa chenye umri wa miaka 33. Mwanzilishi wa chama (Edwin Mtei) alikaa madarakani kama Mwenyekiti kwa miaka 6. Akaondoka, akamkabidhiti shemeji yake. Ndio! Mwenyekiti wa pili wa CHADEMA (Bob Nyanga Makani alioa dadake Edwin Mtei). Makani akakalia kiti miaka 6.

Kisha akamuachia Freeman Mbowe ambaye kakalia takribani miaka 21. Mbowe yeye kaoa mtoto wa Edwin Mtei (Mwenyekiti wa kwanza ambaye ni shemeji wa Mwenyekiti wa pili).

Kwa ufupi, chama chenye umri wa miaka 33 kimekuwa chini ya karibu familia moja kwa miaka yote na kimejenga mifumo na watu kwa mwelekeo wao ikiwemo kumleta hata Lissu CHADEMA, kama ambavyo alisema Mbowe kuwa alimleta Lissu kwenye chama hicho.

Kuchanganyikiwa kwa Lissu kunatoka wapi?

Lissu amechukua chama ambacho anaishi nacho kwa wasiwasi kuwa hakuna wa kumuamini ndani kufanya naye kazi. Anaogopa kila mtu kwa kuwa anajua watu wote wanaomzunguka wamejengwa kama si na Mtei basi na Makani na kama si Makani basi Mbowe, ikiwemo yeye mwenyewe. Ujenzi huo umefanyika katika miaka 33 ya Chadema.

Kingine ni dini. Vita ya Ukatoliki na Uluteri. Yes. Kwa miaka 33 Chadema imekuwa himaya ya Uluteri, viongozi wake wakuu wakiwa Waluteri. Lissu ni Mkatoliki na sasa anaona kazungukwa na masalia ya Uluteri. Kwenye kumsaidia Lissu kufuta mfumo wa Kiluteri Chadema yuko Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki anaitwa Padri Charles Kitima. Huyu ndiye anamsaidia Lissu kusafisha Uluteri.

Hali inavyokwenda itabidi Lissu atafute watu nje ya chama hicho kufanya nao kazi kama ambavyo ameanza lakini hata hivyo hatafanikiwa kwa kuwa wengi wao hawazijui siasa za upinzani nchini. Matokeo yake tumeanza kuyaona kwa kutofanikiwa kwa mambo kadhaa kama kukosa watu kwenye mikutano na kushindwakuchangisha fedha kujiendesha.

Yote kwa yote, katika mazingira haya ni haki yake Lissu kuishi kwa wasiwasi kwani hakika wahafidhina (conservatives) wa CHADEMA hawatasita kuchukua hatua za haraka mambo yakizidi kwenda kombo. Wasiwasi huu wa Lissu maarufu kwa kimombo kama Paranoia utakuwa na madhara makubwa na ndio mwisho wa zama.

Dkt. Hamza Kulanga

Safarini Mutukula