MTIHANI WA KUWA MTOTO WA RAIS NA TUHUMA ZA MANGE DHIDI YA ABDUL.

MTIHANI WA KUWA MTOTO WA RAIS NA TUHUMA ZA MANGE DHIDI YA ABDUL.

Na Mwalimu Hamza Kejo, Mwanza, Tanzania.

Historia huwa inajirudia.. Mnakumbuka enzi Kikwete tulivyoaminishwa kuwa mali zote nchini ni za mwanaye Ridhiwani? Mnakumbuka enzi za Magufuli pale Masaki tulivyoaminishwa nyumba zile mbili kampa mwanaye Jesca? Baadaye huyo huyo Mange akasema Magufuli anaishi na hazina ya nchi chumbani kwake.

Kwamba hazina ya nchi nzima ikae ndani ya chumba cha Rais. Baadaye alifuta post zote chafu dhidi ya Magufuli baada ya mtu mmoja kujitolea kumlipa mamilioni.
Ninachotaka kusema ni kwamba yanayojiri sasa kupitia kwa Mange dhidi ya Abdul si mapya.

Pengine hata nguo tunazovaa iko siku atasema ni mali ya Abdul kama akiona ni post itakayofanikisha malengo yake. Nimewaza kwa nini anafanya haya? Anataka kulipwa kama wakati wa Magufuli au analipwa na mahasimu wa kisiasa wa Rais Samia na Abdul?

Yeyote iwavyo nawapongeza wahusika wote hasa vyombo vya usalama Tanzania na familia ya Rais kwa kuamua kutoendeleza utaratibu wa kuwalipa watu wa aina ya Mange ili tu wasiwabagaze kwa mambo mtandaoni ambayo mara nyingi ni ya uongo mtupu.

Mmeamua kutokuwa mateka kwa kumuacha afanye biashara yake na kusema anachotaka na kwa kuamua kwenu kutokuwa mateka mmewasaidia Watanzania wengine wengi ambao ameharibu na angeharibu maisha yao kwa habari nyingine nyingi za uongo siku zijazo ambazo amekuwa akinunua na kuuza kupitia app yake. Biashara haramu, ya laana na ya kifedhuli sana. Mmefungua mlango wa nchi kupata tiba mtandaoni dhidi ya uongo, uzandiki na uhalifu wa mtandao.