Rais wa aina hii hutokea mara chache sana katika miaka mingi – Sehemu ya Kwanza.

Rais wa aina hii hutokea mara chache sana katika miaka mingi – Sehemu ya Kwanza.

RAIS WA AINA HII HUTOKEA MARA CHACHE SANA KATIKA MIAKA MINGI – SEHEMU YA KWANZA

Na Ngabero Nyangwine, Mara Tanzania

1.⁠ ⁠Rais anayeingia madarakani na kuwa kama amewafungua kutoka utumwani na vitisho vya utawala na kujali misingi ya demokrasia. Ingekuwa mimi mbona mngeisoma namba na mbishi ndugu zake wangemuota kwenye kiroba Coco Beach au angepotea moja kwa moja.

2.⁠ ⁠Rais anayeingia madarakani kuwakumbusha utakatifu wa Katiba mliyo nayo. Bila hii kuna watu hata Katiba hamjui ina mambo gani ya msingi.

3.⁠ ⁠Rais anayeingia madarakani na kuwaambia ukweli. Mkikopa anasema mmekopa, mkitumia chenu anasema mmetumia chenu. Sio mnakopa halafu mnajigamba pesa ni zenu wakati idadi yenu ya walipakodi za maana inahesabika.

4.⁠ ⁠Rais anayeingia madarakani na kusema waziwazi falsafa ya uongozi wake badala ya kwenda na upepo.

5.⁠ ⁠Rais asiyeutaka umungu mtu. Mimi picha zangu mngeweka hadi ndani ya daladala tena kwa lazima. Hata mungu mngeniita kwa bahati mbaya.

6.⁠ ⁠Rais anayeweza kusamehe hata ambao walitamani Katiba ivunjwe ili asipate Urais. Hii ningechinja mtu baada tu ya kula kiapo cha Urais wala hakuna discussion.

7.⁠ ⁠Rais mwanamke ndani ya miaka 63 toka kupata Uhuru. Haitokei mara nyingi. Inawezekana tukapiga miaka mingine kama 50 bila kuona hii ikitokea.

8.⁠ ⁠Rais anayetamka waziwazi kwamba anataka kubadili mfumo wa elimu uwe na faida kwani umepitwa na wakati. Kawaida mtawala angependa watawaliwa wabaki wajinga. Inahitaji neema ya Mungu kuwaza tofauti.

9.⁠ ⁠Rais anayeweza kukusaidia huku unamkosea heshima. Leo unaenda kuomba mchango wa kujenga Kanisa anakupa, kesho unaenda kumtukana hadharani, keshokutwa unarudi kuomba tiba ya mgonjwa wako anakupa.

10.⁠ ⁠Rais aliyeweza kuzipa mashine za MRI hospitali zote rufaa Tanzania ndani ya miaka mitatu kitu ambacho kimesubiri miaka zaidi ya 30.

11.⁠ ⁠Rais ambaye haishi kwa kutaka kusifiwa wala hakosi usingizi kwa wewe kutumia uhuru wako wa kusema na kutoa maoni yako.