Serikali yaleta mikopo nafuu ya riba ya asilimia 7 kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Serikali yaleta mikopo nafuu ya riba ya asilimia 7 kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati.

Serikali imetenga Tsh bilioni 18.5/- za mikopo. nafuu ya kuwezesha wajasiriamali nchini kupitia Benki ya NMB, ambayo itatolewa kwa riba ya 7%.

Mkataba wa utoaji wa mikopo hiyo, umetiwa saini tarehe 6 May 2024 Jijijni Dar es Salaam na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ruth Zaipuna na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Seif Shekalaghe.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, wafanyabishara wadogo na wa kati watakopeshwa fedha hizo kupitia benki hiyo kwa riba ya asilimia 7.

Dkt. Gwajima amesema kwamba fedha hizo ni sehemu ya utaratibu wa serikali, wa kuwezesha makundi maalumu na kuhakikisha wanufaika wake ni wale tu waliolengwa kupata usaidizi huo.

“Wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wana mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, kwa hiyo kuwakwamua na kuwachezesha ikiwemo kupata mikopo hii nafuu ambayo NMB imeanza kuitoa leo (jana)”, alisema Dkt. Gwajima.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benk hiyo, Ruth Zaipuna alisema mkataba wa kutoa mikopo hiyo ni kielelezo cha jitihada zinazofanywa na benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita, za kuboresha mazingira ya biashara changa, ndogo na za kati chini.