Tarehe muhimu katika historia ya CHADEMA ikiendelea kujitetea kutokuwa chama cha kidini wala kikabila.

Tarehe muhimu katika historia ya CHADEMA ikiendelea kujitetea kutokuwa chama cha kidini wala kikabila.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilianzishwa miaka 32 iliyopita yaani mwaka 1992.

Viongozi waasisi wa Chadema ni pamoja na Ndugu Edwin Mtei aliyekuwa Gavana wa Banki Kuu (Baba Mkwe wake Mwenyekiti wa sasa, Bwana Freeman Mbowe), Brown Ngululupi, Dr Amani Walid Kabourou, Ndesamburo na wadau wengine.

Suala la udini na ukabila limeendelea kuwa mwiba kwa CHADEMA hasa kuendelea kuwepo madarakani kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ambaye ni mkwe wa muasisi wa chama hicho, mzee Edwin Mtei. Tuhuma za ukabila na udini zimeendelea kuikumba CHADEMA ambako pia kwa kiasi kikubwa kwenye mitandao ya kijamii maoni na wengi wanaokiunga mkono wanaelekea kuwa watu wa dini moja au ukanda mmoja wa nchi kutoka na utafiti wa majina ya ukoo na majina ya mwanzo.

Mbali na vigingi vyote hivyo CHADEMA imeendelea kukanusha tuhuma hizo.

Tarehe muhimu

  • Mei 28 mwaka 1992 – Kuanzishwa
  • Mwaka 1995 Chadema ilipata wabunge 4 na madiwani 42
  • Mwaka 2000 Chadema ilipata wabunge 5 na Madiwani 75;
  • Mwaka 2005 Chadema ilipata wabunge 11 na madiwani 103;
  • Mwaka 2010 Chadema ilipata wabunge 49 na madiwani 467; hapo bila kuongeza chaguzi ndogo.

Tuhuma za mfumo wa kindugu kwenye uongozi

Mwenyekiti wa kwanza ni Edwin Mtei (1992 hadi 1992) anatokea Kilimanjaro. Mwenyekiti wa pili Bob Nyanga Makani (Shemeji yake Mwenyekiti wa kwanza/Alimuoa mdogo wake Edwin Mtei), alikuwa Mwenyekiti kuanzia mwaka 1998 hadi 2003. Mwaka 2003 hadi leo Mwenyekiti ni Freeman Mbowe ambaye ni mkwe wa Mwenyekiti wa kwanza.

Pengine huu ni wakati wa CHADEMA kujitafakari upya kama kweli inataka kufanya siasa za ukombozi ama siasa za ujasiriamali.