Kuanzia mwaka 2019, jina Kigogo2014 lilijipatia umaarufu mkubwa na wafuasi wengi wa mtandaoni nchini Tanzania. Kigogo2014 ambaye jina lake halisi ni Didier Mlawa alijizolea umaarufu huo kwa machapisho yake ya utetezi wa demokrasia, haki za binadamu na ubadhirifu chini ya utawala wa Rais John Magufuli. Uanaharakati wake huo ukamjengea maadui wakubwa kwenye utawala wa Magufuli...
