Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, amesema uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Deogratius Ndejembi kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais.
Uteuzi wake ulifanyika Agosti 26, 2026 na kuthibitishwa na Bunge Agosti 28, 2026.
